Monday, August 4, 2014

Van Gaal: ‘Nitawaambia usoni nyota wasiohitajika United

Wachezaji wa Man United wakiwa wanajipanga kwa ajili ya kufanya mazoezi wakijiandaa na mechi ya fainali ya Guinness Championship Cup ambapo watacheza na Liverpool leo mjini Miami.
Wachezaji wa Man United wakiwa wanajipanga kwa ajili ya kufanya mazoezi wakijiandaa na mechi ya fainali ya International Champions Cup ambapo watacheza na Liverpool leo mjini Miami.
Kocha wa Manchester United atawaambia wachezaji wake usoni kama hawana faida tena United baada ya ziara ya klabu hiyo kumalizika nchini Marekani ili kukubaliana nao waondoke Old Trafford.
Anderson, Nani, Javier Hernandez, Shinji Kagawa na Marouane Fellaini ni miongoni mwa majina makubwa yaliyo hatarini kuondolewa kabla ya mwisho wa uhamisho.
“Nitatoa hukumu baada ya hii ziara, alisema. “Nimewaacha wote wacheze ila kwa sasa najua zaidi kabla ya ziara.”
“Muda wa kutoa hukumu bado ila katika soka huna budi kuhukumu. Unatakiwa kumpa mchezaji nafasi ya kuhama ikiwa unaona maendeleo yake ya kucheza yanapungua.”
“Unapaswa kulisema hili mapema kwa sababu tutachelewa kabla ya Agosti 31. Nitawaambia wachezaji baada ya ziara ila sio nyinyi.”

No comments:

Post a Comment