Monday, August 4, 2014

Madrid wakamilisha usajili wa Navas.


Hatimaye Real Madrid wamefanikiwa kumpata mlinda mlango mpya Keylor Navas 27 kutoka katika klabu ya Levante kwa ada ya uhamisho wa pauni 7.9m (Tshs bil 19.75).

Kipa huyo alipata umaarufu katika michuano iliyopita ya Kombe la Dunia kwa kukiwezesha kikosi chake cha Costa Rica kufikia hatua ya robo fainali kabla ya kutolewa na
Uholanzi katika hatua ya hiyo kwa mikwaju ya penati.
kip1
Tayari Navas ameshatilia sahihi mkataba wa miaka sita katika kikosi hicho cha Los Blancos na anatarajiwa kuweka upinzani mkali kwa makipa wa klabu hiyo kama,
Iker Casillas na Diego Lopez kwa msimu mpya wa 2014/2015.

No comments:

Post a Comment